Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuwalisha watu milioni 3.5 Korea Kaskazini

WFP kuwalisha watu milioni 3.5 Korea Kaskazini

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linazinduia oparesheni ya dharura ya lishe na chakula ili kutoa huduma kwa watu milioni 3.5 wanaokabiliwa na njaa nchini Korea Kaskazini.

Oparesheni hiyo ambayo itakuwa na usimamizi wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa chakula kimewafikia waathirika itaegemea zaidi lishe ya wanawake na watoto.

Kulingana na uchunguzi ulioongozwa na WFP ulionyesha kuwa uhaba wa chakula nchini Korea Kaskazini umesababisha kuzorota kwa afya miongoni mwa mamilioni ya watu wanaotafuta njia za kujilisha . Emilia Casella ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)