Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano nchini Libya yamezidhisha adha kwa raia

Mapigano nchini Libya yamezidhisha adha kwa raia

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mapigano yanayoendelea katika eneo la Dehiba kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia yamewazuia wakimbizi wanaokimbia kutoka magharibi mwa Libya likisema kuwa huenda wakimbizi hao wamejipata kati kati mwa mapigano kati ya serikali na wanaoipinga serikali.

Kulishuhudiwa milolongo mirefu ya magari yaliyo na wakimbizi kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia kabla ya kuchacha kwa mapigano hiyo jana baada ya zaidi ya watu 3000 kuvuka mpaka siku ya Jumatano.

Hata hivyo awamu ya sita ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ya kuwahamisha wakimbizi kutoka mji uliokumbwa na mapigano nchini Libya wa Misrata inaendelea kwenye mji wa Benghazi. Jumbe Omari Jumbe ni kutoka shirika la IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)