Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika yasaidie kupambana na ufisadi:UNODC

Mashirika yasaidie kupambana na ufisadi:UNODC

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC ametoa wito kwa sekta za umma na za kibinafsi kwenye nchi zilizostawi duniani kuchukua hatua ambazo zinaweza kuangamiza ufisadi akisema kuwa suala hilo linaweza kuzua mizozo.

Yury Fedotov amesema kuwa yaliyotokea hivi majuzi kwenye mataifa ya kaskazini mwa Afrika na mashariki ya kati ni ishara kuwa ufisadi una nguvu za kuleta msukosuko katika jamii.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili mjini Paris ulio na kauli mbiu kuungana dhidi ya ufisadi Fedotov amesema kuwa hata kwenye maeneo yaliyo na amani na maendeleo ufisadi unaweza kuwa tisho kubwa.