Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ya jinsi itakuwa rahisi ikifanywa kuwa lazima:UM

Elimu ya jinsi itakuwa rahisi ikifanywa kuwa lazima:UM

Utafiti ulioendeshwa na Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa programu za elimu ya ujinsia kwa vijana zitakuwa za gharama ya chini ikiwa zitaunganishwa na kufanywa kuwa za lazima.

Utafiti huo unaonyesha kuwa ikiwa programu hizo zitapangwa kwa njia bora gharama ya kila mwanafunzi itakuwa dola 6.90 nchini Nigeria hadi dola 32.80 nchini Uholanzi kulingana na matokeo yautafiti kwenye nchi sita ulitolewa na shirika la elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

Mratibu wa masuala ya virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi kwenye shirika la UNESCO Mark Richmond anasema kuwa utafiri huo unatoa ufahamu zaidi katika kuwekeza katika programu za elimu ya ujinsia kwenye mashule hasa kwenye nchi zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi.