Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unatumia mitandao ya kijamii zaidi kueneza ujumbe wake

UM unatumia mitandao ya kijamii zaidi kueneza ujumbe wake

Umoja wa Mataifa kupitia kitengo chake cha upashaji habari, DPI kimeendelea kuongeza uwigo wa kutumia vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba masuala muhimu yanayohusu umoja huo yanasambazwa kadri inavyotakiwa ulimwenguni kote.

Kwa mujibu wa mkuu wa masuala ya habari na mawasilino wa Umoja wa Mataifa Kiyo Akasaka, amesema kuendelea kushamiri kwa mitandao ya habari ya kijamii kumezidi kuongeza fursa kwa wananchi kufaidika na mambo mbalimbali ambayo umoja wa mataifa inayapigia kifua.

Ametolea mfano yale yaliyojiri hivi karibuni huko Kaskazini mwa afrika na mashariki ya kati ni ushahidi tosha unaodhihirisha namna mitandaa ya kijamii ilivyokuwa na ushawishi mkubwa.

Ameeleza kuwa kukua kwa kasi kwa sekta ya habari na mawasiliano hasa katika nyakati hizi ambazo matumizi ya Internet yamekuwa ni jambo lisilokwepeka tena,kunaongeza msukumo wa umoja wa mataifa kuendelea kujikita kwenye sekta hizo ili hatimaye kufanikisha malengo ya umoja huo yanayohusu maeneo mbalimbali .