Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu Sahara Magharibi zinapaswa kulindwa:UM

Haki za binadamu Sahara Magharibi zinapaswa kulindwa:UM

Kutokuwepo kwa mamlaka toka kwa ujumbe wa umoja wa mataifa kwenye eneo la Sahara Magharibi ili kuangazia hali ya haki za binadamu kumeelezewa na mwakilishi wa umoja huo huko Afrika kusini kuwa ni kama " dhihaka."

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la usalama, Balozi Baso Sangqu amesema kuwa baraza hilo la usalama limeshughulia hali ya mambo katika nchi za Libya na Ivory Coast kwa uharaka zaidi, lakini limezembea kuchukua hatua kama hizo huko Sahara Magharibi.

Ametaka kuchukua mkondo wa jinsi hiyo hiyo katika eneo hilo ili kuhakikisha kwamba haki za wananchi wa eneo hilo zinaheshimika na kulindwa.

Amesisitiza kuwa kama ilivyobainishwa kwenye tamko la kimataifa la haki za binadamu kuwa kila binadamu anayo haki ya kufarahia haki ya kuishi na mambo mengine, hivyo Umoja wa Mataifa inajukumu la kuhakikisha kwamba haki hiyo inapatikana.