UNESCO imelaani mauaji ya mkurugenzi wa habari Bolivia

28 Aprili 2011

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ameitaka serikali ya Bolivia kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji ya kikatili ya David Nino de Guzman aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la habari la Bolivia.

Guzman alikutwa amekufa eneo la Restamanis mjini La Paz Aprili 21 siku mbili baada ya kuripotiwa kwamba hajulikani alipo. Kwa mujibu wa kamati ya kulinda waandishi wa habari mkurigenzi huyo aliuawa kwa kulipuliwa na bomu.

Bi Bokova amelaani vikali mauaji hayo na amesema kwa serikali ya Bolia kuchunguza mazingira ya kifo chake na kuwaadhibu waliomuua kutatoa ishara muhimu kwamba uhuru wa kujieleza ni haki, na uhuru wa vyombo vya habari unawajibu mkubwa wa kuielimisha jamii.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter