Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF imesaidia mamilioni ya watu mwaka 2010:UM

CERF imesaidia mamilioni ya watu mwaka 2010:UM

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia masuala ya kibinadamu kwa kuhakikisha msaada wa haraka kwa watu walioathirika na vita na majanga ya asili CERF, mwaka jana ulitenga dola milioni 415 ili kuyawezesha mashirika ya misaada kuwasaidia watu milioni 22 katika nchi 45.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa CERF ilikuwa kiungo muhimu cha msaada kwa karibu kila janga kubwa lililotokea duniani mwaka 2010 na iliziba mapengo ya fedha na kutoa fursa na maelfu ya watu waliohitaji msaada duniani kuweza kusaidiwa.

Karibu dola milioni 52 zilitolewa kwa Pakistan ambayo ilikumbwa na mafuriko ya kihistoria mwezi Julai mwaka jana na kuifanya kuwa nchi iliyopokea msaada mkubwa kabisa wa CERF 2010, ikifuatiwa na Haiti, Niger, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)