Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua njia za kusafirisha maji Darfur

UM wazindua njia za kusafirisha maji Darfur

Kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na kile cha muungano wa Afrika cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur cha UNAMID kimeanzisha mPango wa kuhakikisha kuwa wenyeji wa jimbo hilo wamepata maji kwa njia rahisi.

Kupitia mpango huo maelfu ya vifaa vya kuhifadhi maji ambapo kila kimoja kina uwezo wa kuhifadhi lita 75 za maji vitasambazwa kwa wanavijiji kwa muda wa majuma mawili yajayo. Wanawake na watoto ndio huwa na jukumu la kutafuta maji kwa familia zao kwenye jimbo la Darfur eneo ambalo hupokea kiasi kidogo cha mvua na mara kwa mara hukumbwa na ukame.

Mkuu wa kikosi cha UNAMID Ibrahim Gambari anasena kuwa moja ya sababu zinazochangia mizozo kwenye jimbo la Darfur ni maji na kuongeza kuwa moja ya malengo yao ni kuzisaidia familia zinazorejea makwao.