Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muongo wa kushughulikia usalama barabarani wazinduliwa:UNECE

Muongo wa kushughulikia usalama barabarani wazinduliwa:UNECE

Mkutano wa uzinduzi rasmi wa muongo wa hatua dhidi ya usalama barabarani katika majimbo ya nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki UNECE umeanza leo mjini Belgrade Serbia.

Mkutano huo utajadili masuala nyeti ya usalama barabarani yanayohitaji kushughulikiwa katika kanda ya UNECE kwa muongo ujao na jukumu la mashirika yanayohusika na masuala ya usalama barabarani katika mchakato huo.

Katika ufunguzi wa mkutano huo katibu mtendani wa UNECE Jan Kubis amesema kuimarisha usalama barabarani ni muhimu sana kwa jamii na ni suala linalopewa kipaumbele na Umoja wa Mataifa. Amesema kuna haja ya kuelimisha jamii, kuichagiza, kuchukua hatua na kufanya mabadiliko endapo watu wanataka kuona hatua zimepigwa katika sula hilo.

Mawaziri kutoka Belarus, Ugiriki, Urusi na Serbia pia wamehudhuria mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 100, kutoka sekta za umma, za binafsi, mashirika ya kitaifa na kimataifa, NGO's na wanazuoni ambao watabadilishana mawazo za mipango madhubuti na sera ambazo itabidi zitekelezwe. Pia wanajadili athari za kijamii, kiuchumi na kiafya zinazosababishwa na usalama mdogo barabarani.