Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wanakutana kwenye kongamano la UM kukabili tishio la maradhi ya moyo, saratani na kiharusi

Wataalamu wanakutana kwenye kongamano la UM kukabili tishio la maradhi ya moyo, saratani na kiharusi

Vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio vinavyoongoza duniani hii leo na vinaongezeka kila siku kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa leo ya shirika la afya duniani WHO kuhusu hali ya magonjwa hayo.

Ripoti hiyo inasema mwaka 2008 watu milioni 36.1 walifariki dunia kutokana na magonjwa hayo kama ya moyo, shinikizo la damu, maradhi sugu ya mapafu, saratani na kisukari. Paul Gawood ni afisa wa WHO

(SAUTI YA PAUL GARWOOD)

Akizindua ripoti hiyo mjini Moscow Urusi mkurugenzi mkuu wa WHO Margaret Chan amesema ongezeko la maradhi yahoo linatoa changamoto kubwa, kwa baadhi ya nchi ni janga kubwa la kiafya, na kiuchumi. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)