Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zahma ya mtambo ya nyuklia Chernobly Ukraine yakumbukwa leo kwenye UM, ni miaka 25

Zahma ya mtambo ya nyuklia Chernobly Ukraine yakumbukwa leo kwenye UM, ni miaka 25

Zahma ya mtambo wa nyuklia iliyotokea Ukraine mika 25 iliyopita leo imekumbukwa katika hafla maalumu kwenye Umoja wa Mataifa.

Hafla hiyo ilianza kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, na maafisa wa kutoka Belarus, Ukraine na Urusi kupiga kengele maalumu ya amani. Kisha kukawa na dakika moja ya ukimya kuwakumbuka maelfu ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo mbaya kabisa ya nyuklia kuwahi kutokea.

Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano maalumu wa kumbukumbu hiyo Ban ambaye ndio kwanza amerejea kutoka Ulaya Mashariki amesema kusoma kuhusu Chernobly ni jambo moja, na kujionea eneo hilo lililoathirika vibaya na nyukia ni sula jingine.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Katibu Mkuu amesema zahma ya Chernobly pia ilikuwa ni hadithi kubwa inayotia matumaini ya mshikamano. Dunia iliungana kusaidia kukabili janga hilo la kihistoria.