Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makundi yenye silaha CAR yazidi kutumia watoto jeshjini:UM

Makundi yenye silaha CAR yazidi kutumia watoto jeshjini:UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Umoja imeelezea jinsi watoto wanavyoendelea kuingizwa jeshini na makundi yaliyojihami katika Jamhuri ya Afrika ya kati na kutoa wito kwa hatua kuchukuliwa kuzuia vitendo hivyo.

Kwenye ripoti hiyo ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la watoto na mizozo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa kati ya masuala yanayochangia kuingizwa kwa watoto jeshini ni pamoja na mapigano ya mara kwa mara kati ya serikali na makundi yaliyojihami, uhalifu uliokithiri na umaskini.

Kwenye ripoti hiyo ya kati ya mwaka 2008 na 2010 Ban anasema kuwa hata baada ya jitihada za serikali za kukomesha kuingizwa kwa watoto jeshini bado makundi ya waasi yanazidi kuwaajiri watoto. Ripoti hiyo inaelezea uovu mwingine ukiwemo mauaji ya watoto , ubakaji , uvamizi kwenye vituo vya afya na kuzuia kutolewa kwa huduma za kibinadamu.