Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu kuhusu haki kwa Wapalestina azuru Mashariki ya Kati

Mtaalamu kuhusu haki kwa Wapalestina azuru Mashariki ya Kati

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika eneo la Wapalestina linalokaliwa tangu mwaka 1967 Richard Falk yuko ziarani katika eneo hilo la Mashariki ya kati tangu jana hadi Mai 3.

Wakati wa ziara yake itakayojumuisha pia nchi za Misri na Jordan, mwakilishi huyo maalumu atakutana na maafisa wa serikali, watetezi wa haki za binadamu, mashirika ya Umoja wa Mataifa, jumuiya za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Hata hivyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo la Gaza, mjumbe huyo amelazimika kuifuta ziara yake kwenye eneo hilo, lakini amehaidi kuelekea huko baadaye mwaka huu. Lakini anaelekea huko Cairo na Amman, ambako anatazamiwa kupata picha halisi namna mwenendo wa haki za binadamu unavyokwenda katika maeneo ambayo yamepokwa toka kwa Palestina.

 

Mtaalamu huyo ambaye shabaya yake kubwa ni kukusanya taarifa mbalimbali kuhusiana na haki za binadamu kabla ya kuweka kwenye ripoti yake itakayotolewa baadaye mwaka huu,hata hivyo amekuwa akipata wakati mgumu toka kwa serikali ya Israel ambayo daima imegoma kutoa ushirilkiano tangu kuteuliwa kwake May 2008.