Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inaendelea kuhamisha wahamiaji Misrata

IOM inaendelea kuhamisha wahamiaji Misrata

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaendelea na shughuli ya kuwalinda na kuwahamisha wahamiaji waliokwama nchini Libya.

Kwa mujibu wa shirika hilo hadi sasa limekwisha hamisha watu 4100 na wengi wao ni wahamiaji kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, Asia na Mashariki ya Kati.

Shirika hilo limeongeza kuwa hofu yake kwa sasa ni mapigano makali yanayoendelea mjini Misrata, idadi kamili ya raia waliokufa na kujeruhiwa haijulikani lakini baadhi ya duru zimesema takribani 300 wameuawa na zaidi ya 1000 kujeruhiwa tangu Aprili 18. jumbe Omari Jumbe ni afisa wa habari na mawasiliano wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)