Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi unawafikia maelfu ya waliokwama Misrata:UNHCR

Msaada zaidi unawafikia maelfu ya waliokwama Misrata:UNHCR

Msaada zaidi wa kibinadamu unawafikia raia waliokwama mjini Misrata Libya kutokana na machafuiko yanayoendelea umesema Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kwamba licha ya msaada huo hali bado ni mbaya.

Duru za hospitali zimeuambia Umoja wa Mataifa watu takribani 300 wameuawa na zaidi ya 1000 kujeruhiwa kati ya Ijumaa iliyopita na Jumapili.

Ndege ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR imewsili mjini Benghazi ikiwa imesheheni msaada ikiwa ni pamoja na mahema 21, vyombo vya jikoni na maplastiki ya kuezekea kwa ajili ya malazi.

Msaada huo utagawanywa kwa wale wanaouhitaji na familia za wakimbizi wa ndani, wanaoomba hifadhi na wakimbizi wengine kwenye miji ya Benghazi, Ajdabiyya na Misrata. Andrej Mahecic kutoka UNHCR anaelezea hali halisi ya Misrata.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECHIC)

Nayo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema watu 9870 wamehamishwa hadi sasa kutoka mjini Misrata, hata hivyo wengine 4700 wengi wao wakiwa wahamiaji bado wamekwama mjini humo.