Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfanyikazi wa WFP auawa Sudan Kusini

Mfanyikazi wa WFP auawa Sudan Kusini

Mfanyikazi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ameuawa katika eneo la Sudan Kusini baada ya kile kinachotajwa kama uvamizi.

Naibu afisa mkuu wa mipango kwenye shirika hilo Santino Pigga Alex Wani alikuwa kwenye shughuli za kikazi pale gari alimokuwa liliposhambuliwa kwenye jimbo la Jonglei tarehe 22 mwezi huu.

WFP imekuwa ikitoa misaada ya chakula kwa watu milioni 1.5 katika eneo la Sudan Kusini na pia kusaidia jamii kurejea maisha ya kawaida baada ya miaka mingi ya mapigano na mizozo. Amemuacha mjane na watoto wawili.