Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya UM vyaanza kusafisha masalia ya silaha Ivory Coast

Vikosi vya UM vyaanza kusafisha masalia ya silaha Ivory Coast

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vimeanza operesheni ya kusafisha

na kukusanya silaha na vifaa vingine hatarishi nchini Ivory Cost kufuatia

kumalizika kwa kipindi cha uhasama kilichoduma kwa miezi kadhaa.

Hali ya sintofamu iliyosababishwa na uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi Novemba, imesababisha mamia kadhaa kupoteza maisha na huku idadi kubwa wakikimbilia katika nchi za jirani. 

Vikosi hivyo UNOCI vimeanza kukusanya silaha ndogondogo, mabomu pamoja na yale ya kutengwa ardhini ambayo yamesambaa kwenye maeneo mbalimbali.

 

Ili kufanikisha operesheni hiyo, kumeandaliwa hatua mbalimbali ikiwemo kuwekwa kwa namba za simu maalumu ambazo zinawapa fursa wananchi kutoa taarifa yoyote

kuhusiana na silaha wazionazo.