Wahamaiji zaidi wawasili mjini Benghazi

25 Aprili 2011

Meli ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM imewasili kwenye mji wa Benghazi nchini Libya ikiwa na wahamiaji 995 na raia wengine waliojeruhiwa kutoka mji uliokumbwa na mapigano wa Misrata.

Waliokuwa ndani ya meli hiyo ijulikanayo kama Red Star One ni pamoja na raia wa Niger 842 , wahamiaji wengine 9 pamoja na raia wa Libya 17. Kuhamishwa kwa watu hao kunafikisha idadi ya watu waliohamishwa na shirika la IOM kuwa watu 4,100 kutoka mji wa Misrata tangu kuanza kwa programu ya kuwahamisha watu mwezi huu.

Hata kama ripoti zinasema kuwa idadi ya wahamiaji ndani na nje ya bandari ya mji wa Misrata inakadiriwa kuwa watu 1500, kuna ripoti kuwa watu zaidi kutoka kwa vitongoji vilivyo magharibi mwa mji huo wanaelekea bandarini. IOM imekuwa kwenye mstari wa mbele katika kuhamishwa wahamiaji ambapo imewasadia wahamiaji 117,000 kurudi makwao na wengine kwenda Misri na Tunisia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter