Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azitaka Cambodia na Thailand kusitisha mapigano

Ban azitaka Cambodia na Thailand kusitisha mapigano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anasumbuliwa na ripoti za mapigano mapya yaliyodumu kwa muda wa siku mbili zilizopita kati ya wanajeshi wa Cambodia na Thailand kwenye mpaka kati ya nchi hizo ambapo watu wengi wameuawa.

Hekalu la Preah VihearBan amezitaka pande hizo mbili kuchukua hatua mwafaka na kusitisha mapigano hayo. Kupitia kwa msemaji wake Ban amesema kuwa mzozo uliopo kati ya nchi hizo hauwezi kutatulia kwa njia za kijeshi ambapo amezitaka pande husika kufanya majadiliano ili kupata suluhu la kudumu. George Njogopa na taarifa kamili:                                                                        (SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)