Mkuu wa UNESCO ataka mjadala juu ya hamta ya uchapishaji

Mkuu wa UNESCO ataka mjadala juu ya hamta ya uchapishaji

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na hali ya kuhifadhi utamaduni wa enzi

limetoa mwito wa kufanyika mjadala kwa shabaya ya kujadilia hali ya uchapishaji

vitabu dunini na kuwepo kwa hati miliki, likisema kuwa mabadiliko ya

teknoolojia yanayoendelea sasa yanaakisi mambo mengi kwenye sekta hiyo.

Kulingana na mkuu wa shirika hilo UNESCO Irina Bokova, kuendelea kuibuka kwa teknolojia za kisasa kumezusha hali ya sintofahamu na kuwaathiri kwa kiwango kikubwa wachapishaji wa vitabu, watunzi na wasomaji wake.

 

Amesema kuna haja ya kufanyika kwa mjadala maalumu ambao utazingatia mambo mengi ikiwemo suala lilohusu hati miliki.

 

 Mkuu huyo ambaye alikuwa akizungumza sambamba na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki miliki, amesema kuwa kwa kutambua changamoto zinazoendelea kuibuka sasa, shirika hilo la kimataifa linatazamiwa kuwa na kongamano maalumu litakalofanyika June mwaka huu huko Monza, Italy ambako mambo mbalimbali yanayohusu mustakabala wa fasii andishi na simulizi itajadiliwa