Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kikanda kuvikabili vitisho ni muhimu:Ban

Ushirikiano wa kikanda kuvikabili vitisho ni muhimu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kuwepo kwa mashirikiano ya

karibu zaidi baina ya umoja huo na washirika wake wa kikanda wanaohusika na usalama ili kufanikisha azma ya kukabiliana na matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu na uhalifu wa kimataifa.

Akiweka msisitizo zaidi juu ya hali hiyo, Ban amesema pande hizo zinapaswa kufanya kazi ili kusukuma mbele majukumu ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani .

 

Ban ambaye alikuwa akizungumza kwenye kongamano la kikanda kwa taasisi za kiusalama huko Moscow, Russia amesema ulimwengu unaendelea kushuhudia kuinuka kwa matukio yasiyotarajiwa ambayo yanazua kitisho kikubwa kwa usalama wa dunia, hivyo ametaka kuwepo kwa mafungamano ya karibu kwa pande zote.

 

Jumuiya hiyo ya kikanda inajumuisha nchi za Armenia, Belarus, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Russia, Tajikistan na Uzbekistan.