Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atao wito wa kutaka kusitishwa ghasia dhidhi ya maandamano ya amani nchini Syria

Ban atao wito wa kutaka kusitishwa ghasia dhidhi ya maandamano ya amani nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameshutumu vikali ghasia zinazozidi kuendeshwa dhidi ya waandamanaji wanaoandamana kwa amani nchini Syria hali ambayo imesababisha kutokea vifo na majeraha mengi na kuutaka utawala wa nchini hiyo kuheshimu sheria za kimataifa na kusitisha umwagaji wa damu.

Kwenye habari iliyotolewa kupitia kwa msemaji wake Ban amesema kuwa kunahitajika kuwe na uchunguzi ulio huru na wenye haki kuhusiana na mauaji hayo ambapo ameutaka utawala wa Syria kulinda haki za binadamu ikiwemo haki ya uhuru wa kusema , kukutana na pia haki ya vyombo vya habari. Vyombo vya habari pia vinaripoti kuwa watu kadha waliuawa siku ya ijumaa wakati maelefu ya watu walipoingia mitaani kwenye miji kadha nchini Syria wakiitisha mabadiliko ya kisiasa.

yria mpaSyria