Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ameitolea wito Urusi kuendelea kuunga mkono UM

Ban ameitolea wito Urusi kuendelea kuunga mkono UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitolea wito Urusi kuendelea kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa za kurejesha amani na utulivu katika maeneo yenye migogoro duniani.

Akizungumza mjini Moscow baada ya mkutano na Rais wa Urusi Ban amesema ni muhimu kwa Urusi kuusaidia Umoja wa Mataifa kufikia alichokiita ajenda ya pamoja. Ban ametaja matukio yanayoendelea kwenye ulimwengu wa Kiarabu kama mfano mmoja.

Amesema machafuko yanayoshuhudiwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini yanadhihirisha haja ya watu kila mahali duniani ya kuishi kwa uhuru, wakiwa na matumaini na kuthaminiwa utu wao.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi pamoja na nchi wanachama ili kutoa msaada wowote wa muhimu unaohitajika kwa watu wanaotaka kuwa na uhuru wa kweli, demokrasia na haki ya maisha ya baadaye.