Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi mpya za bunge la Haiti zafunguliwa:UM

Ofisi mpya za bunge la Haiti zafunguliwa:UM

Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti Edmond Mulet amemkabidhi spika wa bunge la Haii funguo za afisi mpya ambazo zitakuwa makao ya bunge kwa muda kando la yaliyo majengo ya bunge yaliyoaharibiwa na tetemeko la ardhi mwaka uliopita.

Afisi hizo za muda ambazo zina nafasi wanayoweza kuketi zaidi ya watu 400 wakiwemo wabunge na maafisa wengine serikalini na pia kwa mikutano zimegharibu karibu dola 700,000 zilizotolewa na shirika la MINUSTAH.

Kwenye sherehe hizo mulet aliwatakia heri wabunge wapya nchini Haiti na awamu yenye manufaa ambapo pia aliwataka kuunga mkono masuala ya uchumi, ya kijamii na kidemokrasia nchini mwao.