Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukosekana hatua za haraka Abyei kunatishia usalama:UM

Kukosekana hatua za haraka Abyei kunatishia usalama:UM

Kukosekana utashi wa haraka Abyei kunaweza kuleta kitisho cha usalama kwenye eneo nzima.

Kumekuwa taarifa za kuzorota kwa hali ya mshikamano katika jimbo la Abyei  nchini Sudan na kuzusha kitisho cha kusambaa kwa hali ya sintofahamu hadi katika maeneo mengine zaidi.

 

Atul Khare ambaye anaongoza vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa amesema kuwa hali ya kuvutana baina ya mamlaka ya Sudan na ile ya Sudan Kusini inazidi kuongeza wasiwasi juu ya mustakabali wa eneo hilo.

 

Afisa huyo amesema kuwa mwenendo huu unaweza kuvuruga uhusiano wa mataifa hayo mawili ambayo yanaanza kujiimarisha upya baada ya sehemu ya Sudan Kusini kuwa taifa jipya kufuatia kura ya maoni iliyofanyika mwezi January mwaka huu. Suala la kuwepo kwa kura ya maoni itakayoamua Abyei ijiunge ama Sudan kaskazini ama kusini bado kupatiwa ufumbuzi.