Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yalalamikia mzigo mzito wa wakimbizi wa Somalia

Kenya yalalamikia mzigo mzito wa wakimbizi wa Somalia

Serikali ya Kenya imelitaka shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kuweka kambi ndani mwa Somalia ili kuzuia idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Somalia wanaovuka mpaka na kuingia nchini Kenya.

Katibu katika wizari ya masuala ya ndani nchini Kenya Francis Kimemia amesema kuwa Kenya tayari imewapa makao wakimbizi wengi zaidi katika eneo hilo na kwamba ghasia zinazoendelea kushuhudiwa nchini Somalia zinazidi kuongeza mzigo huo kila kukicha.

Kwa upande wake mwakilishi wa UNHCR nchini Kenya Elike Segbor amesema pendekezo hilo la Kenya litashughulikiwa lakini akaonya kuwa sheria za kimataifa haziruhusu nchi yoyote kuwafungia mipaka wakimbizi. Kulingana na Umoja wa Mataifa hadi sasa kuna wakimbizi 370,000 kutoka Somalia walio nchini Kenya.