Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa surua walikumba bara la Ulaya:WHO

Mlipuko wa surua walikumba bara la Ulaya:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema kuanzia Aprili 18 mwaka huu nchi 33 barani Ulaya zimeripoti visa zaidi ya 6500 ya surua.

Uchunguzi wa maabara na vipimo vingine vimethibitisha kuwa ni maambukizi ya surua katika nchi za Ulaya na Amerika. Hadi sasa Ubeligiji ina wagonjwa 100, Bulgaria 131, Ufaransa 4937, Serbia 300, Granada 250 na Hispania 600. Mlipuko huo umearifiwa pia miongoni mwa wahudumu wa afya pia. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ripoti juu ya ugonjwa huo ambao ulizuka kwa mara ya kwanza Septemba 2010  huko Macedonia zinaonyesha kwamba mamia ya watu wamekumbwa hadi kufikia April mwaka huu.

Nchini Uturuki pekee ripoti zinaonyesha kuwa katika mji wa Istanbul watu 80 wamebainika kukumbwa katika kipindi cha mwezi January. Hali inavyoonekana siyo ya kutia matumaini kwani kumekuwa na ongezeko la wagonjwa katika nchi kadhaa kama Ujerumani, Uholansi, Norway, Uingereza na Urusi.