Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaonya juu ya mlipuko wa polio Ivory Coast

WHO yaonya juu ya mlipuko wa polio Ivory Coast

Ivory Coast inakabiliwa na mlipuko wa virusi vya polio type 3, huku kukiwa na visa vitatu vipya vilivyoripotiwa Januari 27, Februari 24 na Februari 27 limesema shirika la afya duniani WHO.

Shirika hilo linasema virusi vya polio type3 ambavyo vinaweza kusababisha mtu kupooza na viligundulika mara ya mwisho katikati ya mwaka 2008 kaskazini mwa Nigeria. Virusi type3 ni mara ya kwanza kubainika Ivory Coast tangu mwaka 2000.

Mwaka 2008-2009 Ivory Coast ilikumbwa na mlipuko wa polio virusi type1 ambavyo vinalikumba sana eneo la Afrika ya Magharibi. Alice Kariuki anaripoti

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)