Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gharama za dawa za malaria zimepungua Afrika:UM

Gharama za dawa za malaria zimepungua Afrika:UM

Mpango wa kimataifa wa kuhakikisha dawa za kuzuia malaria zinapatikana kwa gharama nafuu katika jamii nyingi za vijiji Afrika unapiga hatua haraka.

Katika nchi za Ghana, Kenya, Madagascar na Nigeria sasa dawa za kutibu malaria zinaweza kununuliwa katika maduka ya dawa na maduka binafsi kwa gharama ndogo ya dola senti 50, ikilinganishwa na mara 20 zaidi kabla ya kuanza kwa mpango huu.

Mpango huu ulianzishwa mwaka jana kwa nchi nane, ambazo ni Ghana, Kenya, Madagascar, Niger, Nigeria, Tanzania, Uganda na Cambodia ili kutoa funzo kabla kuanza dunia nzima, na matokeo yameanza kuonekana hasa katika nchi nne zilizoanza kutekeleza mapema mpango huo.