Skip to main content

Kuilinda dunia kutasaidia kuimarisha uchumi:Migiro

Kuilinda dunia kutasaidia kuimarisha uchumi:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ametoa wito kwa mataifa kuhakikisha kuwa yamepunguza gesi zinazochafua mazingira hasa za Carbon kama moja ya njia ya kuchangia katika maendeleo.

Akiongea kwenye warsha ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya dunia Migiro amesema kuwa ulimwengu unashuhudia mabadiliko makubwa pamoja na maendeleo hasa kwa nchi zinazoinukia kiuchumi kwa muda wa miongo miwili iliyopita.

Migiro pia amesema kuwa mamilioni ya watu barani Asia , Amerika ya kusini na Afrika wamejikwamua kutoka kwenye umaskini akiongeza kuwa watu zaidi wanastahili kupata mafanikio kama hayo.