Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM leo umeadhimisha siku ya lugha ya Kichina

UM leo umeadhimisha siku ya lugha ya Kichina

Umoja wa Mataifa leo umeadhimisha siku ya lugha ya Kichina kama sehemu ya juhudi za Umoja huo kutanabaisha umuhimu wa historian a utamaduni katika lugha sita ambazo ni rasmi kwenye Umoja wa Mataifa.

Maadhimisho hayo yameambatana na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na warsha za kuandika Kichina, sarakasi, muziki na ngoma za asili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Siku ya leo iliteuliwa na Umoja wa mataifa kumuenzi Cang Jie mtu anayedhaniwa kuanzisha tarakimu na maandishi ya Kichina takriban mika 5000 iliyopita. Kichinina ni moja ya lugha za zamani sana duniani ikikisiwa kuanza miaka 4000 iliyopita na sasa inazungumzwa na watu zaidi ya bilioni moja duniani.