Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa UM kupambana na uharamia kupata dola milioni 5

Mfuko wa UM kupambana na uharamia kupata dola milioni 5

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na uharamia pwani ya Somalia umeahidiwa dola zaidi ya milioni 5 katika siku ya mwisho ya mkutano wa kupambana na uharamia uliokamilika mjini Dubai.

Ahadi hizo ni pamoja na dola milioni moja zilizoahidiwa na serikali ya Emarati. Wengine walioahidi ni kampuni ya masuala ya bandari ya Abu Dhabi, serikali ya Uholanzi, Norway, Ufaransa na Korea ya Kusini. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga aliyehudhuria mkutano huo anasema kuwa anatarajia fedha zaidi kutolewa.

Pia kwenye mkutano huo kuliafikia makubaliano ya kuhamishwa kwa maharamia waliohukumiwa kati ya ushelisheli na Somalia makubaliano yaliyotiwa sahihi na waziri wa masuala ya ndani wa ushelisheli Joel Morgan na waziri anayehusika na masuala ya usafiri wa baharini nchini Somalia Said Mohamed Rage.

Kwa upande mwingine mkutano wa jumuiya ya Afrika Mashariki uliondaliwa nchini Tanzania umeitaka jamii ya kimataifa hasa Muungano wa Ulaya na Marekani kushughulikia tatizo la uharamia na kukiunga mkono kikosi cha kulinda amani nchini Somalia cha AMISON.