Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto walindwe Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini:UNICEF

Watoto walindwe Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini, kuanzia Libya, Yemen, Israel na eneo linalokaliwa la Wapalestina yanaathiri pakubwa maisha ya watoto na vijana.

Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake amezitaka pande zote kuchukua hatua zaidi kuhakikisha watoto wanalindwa katika maeneo hayo kwa kuzingati mkataba wa kimataifa wa haki za watoto.

UNICEF inasema hata kabla ya kuzuka machafuko watoto wengi katika maeneo hayo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto, kwa afya zao na maisha yao kwa ujumla, na ameongeza kuwa sasa wako katika hatari kubwa zaidi kutokana na machafuko yanayoendelea.