Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi Misrata yaweza kuwa uhalifu wa kivita:Pillay

Mashambulizi Misrata yaweza kuwa uhalifu wa kivita:Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amelaani vikali matumizi mabomu mtawanyiko na silaha nzito zinazotumiwa na majeshi ya serikali Libya kwa lengo la kuchukua udhibiti wa mji wa Misrata.

Amesema mashambulizi hayo kwenye maeneo yenye watu wengi , na kusababisha vifo vingi vya raia yanaweza kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za haki za binadamu. Taarifa zinasema bomu moja limeripuka kilometa chache kutoka Misrata hospitali na duru zingine zikisema vituo viwili vya afya vimeshambuliwa.

Hadi sasa idadi kamili ya raia waliokufa na kujeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo haijajulikana. George Njogopa

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)