Wakati zahma ya Chernobly ikikumbukwa Ban ameitaka dunia kujifunza kutokana na ajali za nyuklia

20 Aprili 2011

Miaka 25 baada ya kutokea zahma ya nyuklia ya Chernobly Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye leo amezuru eneo hilo amewakumbuka watu zaidi ya 330,000 waliopoteza maisha yao ikiwa ni pamoja na wafanyakazi 600,000 wa zima moto waliokufa wakijaribu kuokoa ulimwengu na kunusuru maisha ya wengine.

Akizungumza kwenye mkutano maalumu wa miaka 25 baada ya Chernobly , usalama wa baadaye, Ban amesema watu milioni sita bado wanaendelea kuishi katika jamii zilizoathirika na nyuklia Beralus, Shirikisho la Urusi na Ukraine, ambako watoto 6000 walipata saratani.

Amesisitiza kwamba maeneo hayo yanahitaji ujenzi mpya na maendeleo, fursa za kazi, uwekezaji mpya, na kurejesha hadhi ya jamii.

Ameongeza kuwa zahma ya Chernobly na Fukushima Daiichi Japan ni funzo kubwa hivyo kuchagiza matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia pia kuhakikisha usalama ni masuala ya muhimu kwa dunia nzima na sio sera za taifa moja.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter