Skip to main content

Kuna haja ya kuongeza uzalishaji bidhaa Afrika:UNCTAD

Kuna haja ya kuongeza uzalishaji bidhaa Afrika:UNCTAD

Wataalamu kwenye warsha iliyoandaliwa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia wamesema kuwa kuendelea kupanda kwa bei ya chakula na nishati huenda vikakwamisha maendeleo ambayo tayari yameshudiwa kwenye nchi maskini barani Afrika wakiongeza kuwa uchumi wao unastahili kulindwa kutoka na misukusuko hii.

Warsha hiyo ya shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa la UNCTAD inayoangazia masuala ya ukuaji wa uchumi na kupambana na umaskini kwenye nchi maskini barani Afrika iliandaliwa kwa ushirikiano na tume ya uchumi barani Afrika.

Mara nyingi UNCTAD imependekeza kuwa nchi maskini zinahitaji kuimarisha mbinu za kuzalisha aina nyingi ya bidhaa. Warsha hiyo imetajwa kuwa fursa nzuri kwa nchi maskini barani Afrika Kujiandaaa kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi maskini .