Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa kujieleza muhimu Algeria inapofanya mabadiliko:UM

Uhuru wa kujieleza muhimu Algeria inapofanya mabadiliko:UM

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki ya kuwa huru na haki ya kusema Frank La Rue amefanya ziara nchini Algeia ambapo alikagua hali ya haki ya kuwa huru na kusema nchini humo.

Mjumbe huyo amesema kuwa Algeria imetoka mbali tangu miaka ya tisini ambapo waandishi 100 wa habari waliuawa. La Rue anasema kuwa kwa sasa waandishi wa habari hawahofii maisha yao wanapotekeleza wajibu wao.

Hata hivyo amesema kuwa waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinatatiza kazi yao. La Rue pia alizungumzia madai kuwa vyombo vya bahari vinavyosimamiwa na serikali viliegemea upande mmoja wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini humo.