Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita vimesambaratisha mfumo wa afya Ivory Coast:WHO

Vita vimesambaratisha mfumo wa afya Ivory Coast:WHO

Kundi moja la wataalamu wa afya kutoka shirika la afya duniani WHO limesema kuwa ghasia za hivi majuzi nchini Ivory Coast zimesambaratisha kwa kiasi kikubwa huduma za afya kwenye maeneo ya magharibii mwa Ivory Coast baada ya ziara ya siku tatu lililofanya katika maeneo ya Moyen Cavally na Montagnes.

Wataalamu hao walizuru vituo vikuu vya kiafya na kukutana na washirika wa kimataifa ili kukagua hali ilivyo na pia kuchunguza vizingiti vinavyowazuia wenyeji kupata huduma za afya.

 Tangu kuanza kwa mzozo nchini Ivory Coast mwezi Disemba mwaka uliopita WHO imekuwa ikitoa huduma za kiafya lakini hata kufuatia kuchacha kwa mzozo kwa muda wa wiki tatu zilizopita kumeifanya WHO kuongeza oparesheni zake . Dr Tarik Jasarevic ni kutoka WHO

(SAUTI YA DR TARIK JASAREVIC)