Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaanza kusafirisha chakula kwenda Libya

WFP yaanza kusafirisha chakula kwenda Libya

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza kusafirisha chakula kwenda magharibi mwa Libya ili kuyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi na mapigano kwa mara ya kwanza kabisa tangu mzozo kuibuka nchini humo.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la WFP Josette Sheeran anasema kuwa ni muhimu kupata njia ya kuwafikia maelfu ya watu walio na njaa waliothirika na mzozo hasa wanawake na watoto na watu wazee ambao wanazidi kupungukiwa na chakula.

Msafara wa kwanza wa malori manane yaliyo na tani 240 za unga wa ngano na tani 9.1 za biskuti vya hali ya juu vyote vilivyo na uwezo wa kulisha watu 50,000 kwa siku 30 yalivuka hiyo jana na kuingia magharibi mwa Libya yakitokea Ras Jedir kwenye mpaka wa Libya na Tunisia. George Njogopa Anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)