Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kusafirisha raia wa Mali waliokwama Ivory Coast

IOM yaanza kusafirisha raia wa Mali waliokwama Ivory Coast

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanza tena kuwakwamua mamia ya raia wa Mali na Mauritania waliokwama nchini Ivory Cost ambako hali ya kisiasa bado haijatengamaa.

Ujumbe wenye mabasi tisa ukiwa umebaba raia 639 wa nchi hizo mbili tayari umewasili katika mji wa Bouke ulioko Kaskazini baada ya kuondoka katika mji mkuu wa Abidjan hapo siku ya jumamosi.

Hili ni zoezi la kwanza kufanywa na shirika hili la kimataifa baada ya kusimamisha huduma zake tangu mwezi March kufuatia kuzuka upya kwa hali ya machafuko kulikotatiza kazi za uokoaji.

Hata hivyo kumeanza kujitikeza kwa hali ya utulivu kwenye maeneo mbalimbali nchini humo jambo ambalo IOM imesema kuwa imekuwa rahisi kwao kuendelea na kazi.