Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Hungary kuhakikisha kuna uhuru wa kujieleza

Ban aitaka Hungary kuhakikisha kuna uhuru wa kujieleza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka serikali ya Hungary kuongeza juhudi katika kuhakikisha uhuru wa kujieleza unapatikana.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Rais Pal Schmitt Ban ameishukuru serikali ya Hungary na watu wake kwa mchango mkubwa wanaoutoa kwenye masuala ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Cyprus, Lebanon , Sahara Magharibi na Afghanistan.

Ban amesema pamoja na juhudi kubwa zinazofanyika nchi hiyo inahitaji kuongeza juhudi zake kwenye uhuru wa kujieleza kwa kufanyia marekebisho sheria za vyombo vya habari ziwe sawa na sehemu zingine za Ulaya.

Ban aliyeko kwa ziara ya siku mbili nchi humo pia amezungumzia sula la Libya na kusema kumekuwa na maafikiano baina ya serikali ya Libya na Umoja wa Mataifa kuruhusu mashirika ya kmisaada ya kibinadamu mjini Tripoli na amesisitiza haja ya kusitisha mapigano yanayoendelea.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)