Skip to main content

Austria yatakiwa kuzingatia haki za binadamu:UM

Austria yatakiwa kuzingatia haki za binadamu:UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki ya utamaduni Farida Shaheed ameishauri serikali ya Austria kuutambua utamuduni na kuuinua kwa kuuunga mkono.

Shaheed amesema kuwa serikali inastahili kushirikisha tamudi za makabila madogo pamoja na historia zao kwenye masomo shuleni, kwenye vyombo vya habari na katika shughuli zingine za kitamaduni.

Hata hivyo amekaribisha hatua zilizopigwa katika kuinua tamaduni mbali mbali lakini akaitaka serikali kuendelea kuinua tamaduni za jamii zingine ndogo nchini humo.