Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 wafa baada ya kuzama Ghuba ya Aden:UNHCR

16 wafa baada ya kuzama Ghuba ya Aden:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa watu 16 wamezama huku wengine watano hawajulikani waliko kufuatia mikasa miwili tofauti kwenye eneo la ghuba ya Aden.

Karibu wote waliozama wanakisiwa kuwa wasomalia waliokuwa wakikimbia ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu nchini mwao. Walionusurika wanasema kuwa wakati wa mkasa huo waliiona meli ya mizigo na nyingine ya kivita ambapo meli hiyo ya kivita ilipuuza ombi lao la kutaka usaidizi.

UNHCR inatoa wito kwa mabaharia kwenye ghuba ya Aden kuitikia wito wa usaidizi baharini ambao umekuwa tangu awali na vyombo vya bahari vinapopatwa na shida.