Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO/WFP wazindua mpango wa huduma za chakula

FAO/WFP wazindua mpango wa huduma za chakula

Mashirika ya Umoja wa Matafia likiwemo shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na lile la mpango wa chakula duniani WFP yamezindua mpango wa chakula wenye lengo la kuimarisha huduma za kusambaza chakula kunapotokea majanga.

Kati ya mashirika yaliyo kwenye mpango huo ni pamoja na shirika la FAO, WFP , mashirika yasiyokuwa ya kiserikali , shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na mashirika mengine ya kibinadamu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kwa mujibu naibu mkurugenzi wa FAO Changchui He, kuwepo kwa mashirika haya ya kirai ikiwemo pia shirika la kimataifa la msalaba mwekundu ni hatua muhimu ambayo itasaidia pakubwa kufanikiwa kwa mpango huo.

 

Kwa upande wake naibu mkurugenzi wa WFP Amir Abdulla amesema kuwa kubuniwa kwa mpango huo ambao unashirikisha wahisani wengi kwa pamoja itatoa mchango mkubwa kunusuru maisha ya watu wanaokabiliwa na tatizo la njaa.

 

Mpango huo wa dharura wa chakula tayari imeanza kufanya kazi katika zaidi ya nchi 25 ambao zimekubwa na majanga ya kimaumbile na kusababisha janga la ukosefu wa chakula.