Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Syria kuacha kuwashambulia raia

UM waitaka Syria kuacha kuwashambulia raia

Kundi moja la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelaani kuongezeka kwa mauaji na mshambulizi yanaoendeshwa dhidi ya waandamanaji , waandishi wa habari na watetesi wa haki za binadamu nchini Syria hata baada ya ahadi ya serikali ya kutekeleza mabadiliko.

Wataalamu hao wamesema kuwa kuna sababu ambazo zinasababisha kutokea kwa maandamano zikiwemo ufisadi , kutokuwepo kwa haki, ubaguzi na kutokuwepo kwa uwajibikaji. Wanasema kuwa mabadiliko ya kisiasa na ya kiuchumi yanahitajika kufanyika kwa haraka.

Wameutaka utawala wa Syria kwa haraka kukomesha ukandamizaji na kufanya majadiliano yaliyo yenye uwazi ili kutekeleza mabadiliko.