Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yahitaji dola milioni 257 kusaidia Waafghanistan

WFP yahitaji dola milioni 257 kusaidia Waafghanistan

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linahitaji kwa dharura dola milioni 257 ili kuendelea kutoa misaada ya chakula kwa watu milioni 7.3 linaolenga kuwasaidia nchini Afghanistan mwaka huu hususan wanawakle na watoto.

Bila ya fedha hizo WFP italazimika kupunguza shughuli na kuwalisha watoto wa shule kwa nusu ifikapo mwezi Juni hali ambayo itawaathiri zaidi ya watoto wa shule milioni moja.

Pia upungufu wa vyakula maalum umeifanya WFP kupunguza idadi ya watoto walio chini ya maiaka mitano inaoweza kuwasaidia kutoka watoto 62,000 hadi watoto 40,000 kila mwezi. Emilia Casella ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)