Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya mkutano na Rais wa Jamhuri ya Czech

Ban afanya mkutano na Rais wa Jamhuri ya Czech

Katibu mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon hii leo amefanya mkutano na rais Vaclav Klaus wa Jamuhuri ya Czech ambapo Ban alimfahamisha yanayojiri katika maeneo ya mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika hasa nchini Libya na Misri.

Ban pia alizungumzia wajibu ambao unaweza kutekelezwa na jumuiya ya Ulaya hasa kwenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mazungumzo baina ya viongozi hao pia yaliguzia maendeleo ya kiuchumi duniani , shughuli za mataifa ya G20 na hali magharibi mwa Balkans.