Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIMIS yakaribisha maridhiano ya kumaliza mzozo Abyei

UNIMIS yakaribisha maridhiano ya kumaliza mzozo Abyei

Ujumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Sudan (UNMIS) amekaribisha hatua zilizochukuliwa za kufikiwa makubaliano ya pamoja kwa pande mbili zinazozana katika jimbo la Abyei ambazo zimeafiki kuunda kamati ya kufuatilia utekelezaji wa maridhiano yanayoyaka vikundi vya waasi kuachana na mienendo korofi.

Zikukutana mjini Khartoum pande zote zimekubaliana kuunda kamati ya kitaalamu ambayo itasimamia utekelezaji wa makubaliano ya Kadugli yaliyofikiwa mwezi January mwaka huu ambayo yalitaka vikundi vyote vya waasi kuachana na mienendo korofi.

Kamati hiyo imepanga kuwa na mkutano wake wa kwanza jumatatu ijayo mjini Abyei na UNMIS imehaidi kupiga jeki ili kufanikisha mkutano huo.Hivi karibuni kwenye eneo hilo kulizuka hali ya sintofahamu kufuatia mkwaruzano ulioibuliwa na pande zote mbili jambo lililopalilia hali ya wasiwasi.