Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT yazindua jumuiya ya mtandao kusaidia miji

UN-HABITAT yazindua jumuiya ya mtandao kusaidia miji

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT limezindua jumuiya mpya ya mtandao iitwayo URBAN GATEWAY ili kusaidia miji na wataalamu wa mipango miji duniani kuungana, kubadilishana uzoefu na kuchukua hatua kwa ajili ya kuwa na miji endelevu katika wakati huu ambapo miji inapanuka kwa kasi duniani.

Wavuti hiyo www.urbangateway.org imezinduliwa na mkurugenzi mkuu wa UN-HABITAT Dr Joan Clos kwenye mkutano wa kimataifa wa baraza la shirika hilo unaofanyika mjini Nairobi Kenya. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Wavuti huo unatajwa kwamba ni jukwaa muhimu likalowawezesha wataalamu wa masuala ya maendeleo miji na vijiji pamoja na watu wa kada nyingine kubadilishana ujuzi na uzoefu juu ya ukongezeko la kasi la miji.

Kulingana na mkuu huyu wa shirika la makazi la umoja wa mataifa Dr Clos ulimwengunu unashuhudia ongezeko la kasi la watu wanahamia kwenye maeneo ya mijini na makadiria ya awali yanaonyesha kuwa kazi hiyo inatazamiwa kuongezeka mara dufu katika siku za usoni.

Hivyo kuanzishwa kwa wavuti huo ambao ni kwanza kuanzishwa juu ya masuala hayo, kunatazamiwa kutoa msaada mkubwa kwa mamilioni ya watu duniani kote.